Usajili Biashara Brela (Jina/Kampuni)

A. JINA LA BIASHARA  (BUSINESS NAME)

Kuna utofauti kati ya kampuni na jina la biashara (business name). Jina la biashara ni jina la utambulisho ambalo umeamua biashara yako ifahamike na kuitwa. Mfano ni majina ambayo wengi wanaandika kwenye maduka yao. Yale ni majina ambayo wameamua duka na biashara zao zitambulike Hivyo. Business name ni jina tu la kufanyia biashara (Brand name).

 Sasa wenye mamlaka ya kusajili majina kwa mujibu wa sheria ni Brela. Na usajili unafanyika kwa njia ya mtandao kupitia https://ors.brela.go.tz/

FAIDA ZA BUSINESS NAME

 • Ukisajili hilo jina unakuwa umelifanya jina la biashara yako litambulike kisheria na kuwa rasmi (kurasimisha).
 • Pia inakusaidia kuweza kuzuia mtu mwingine kutumia jina lako isivyohalali. Mfano ni hatari kulikuza jina ambalo hujasajili, au jina la bidhaa maarufu bila kulisajili hilo jina ili kulinda mtu mwingine adandie brand yako au bidhaa yako.
 • Kwasababu jina linakuwa rasmi, unaweza kufungua account ya bank yenye hilo jina lako ulilosajili. Hii inasaidia katika uaminifu mtu akiona analipa kwenye account yenye jina la biashara.
 • Mtu mmoja au kama mko kikundi mnaweza kusajili jina la biashara, na kikundi chenu kikafahamika kwa hilo jina kiasi kwamba hata account ya bank mnaweza kufungua kwa hilo jina.
 • Pia kama mnataka mikopo kwenye taasisi za fedha huwa wanahitaji usajili wa namna hii kama ushahidi kuwa ninyi ni kikundi halali na sio kikundi hewa ambacho hakijasajiliwa popote.

GHARAMA ZA USAJILI

Kujua gharama angalia brela.go.tz, sehemu ya Business name, the angalia kipengele cha fee structure. Utaona wameweka gharama ya usajili jina brela ni 20,000 (elfu ishirini)

MAHITAJI ILI KUSAJILI

Kwa business name vinavyo vinavyohitajika ni;

 • Namba ya Nida
 • Namba ya simu
 • Barua pepe
 • Sanduku la posta
 • Eneo unaoishi na eneo unapofanyia biashara (Mkoa, Wilaya, Kata, Mtaa, Jirani na kitu gani maarufu

B. KUFUNGUA KAMPUNI

Kufungua kampuni sio lazima uwe na mtaji, na gharama za kufungua ni ndogo sana. Angalia hapa https://www.brela.go.tz/index.php/companies/fees gharama zake zilivyoanishwa na Brela. Lakini faida ya kufungua kampuni ni kubwa sana sana na ni muhimu sana.

Kwa kifupi, ukiwa na kampuni;

 • Makadirio ya kodi utafanya mwenyewe
 • Inatambulika kisheria(legal entity).
 • Kama una hasara hutakiwi kulipa kodi
 • Huwezi kurisisha Kazi ya kuajiriwa, bali unaweza kurithisha Kampuni. Na pia ni rahisi kuepuka migogoro ya mirathi kama una kampuni kuliko mali binafsi
 • Ni rahisi kukopesheka kama biashara iko vizuri au kuaminika na makampuni mengine.
 • Ukiwa na kampuni ni rahisi kutumia mtaji wa kampuni nyingine pasipo mkopo. Yaani ni rahisi kupewa bidhaa na kampuni nyingine pasipo kulipa kwanza kwa makubariano ya kulipa baada ya kuuza (Credit facility).
 • Kwa hiyo ukiwa na kampuni wimbo wa sina mtaji unapotea na pia unaingia kwenye uwanja wa kula vinono. (Mfano huwezi kupata tenda ya kutengeneza barabara kama wewe sio kampuni).

FAIDA ZA KUFUNGUA KAMPUNI KIUNDANI

 • Kuwa na kampuni kunakuwezesha kuingia katika biashara kubwa kubwa ambazo hawezi kupewa mtu binafsi (contract au tenda) na pia inafungua mlango na trust kuweza kushirikiana  na makampuni mengine, kwa kuwa makampuni yanaamini na kufanya biashara na makampuni badala ya mtu binafsi.
 • Pia ukiwa na kampuni ni rahisi kutumia mtaji wa kampuni nyingine pasipo mkopo. Yaani ni rahisi kupewa bidhaa na kampuni nyingine pasipo kulipa kwanza kwa makubariano ya kulipa baada ya kuuza (Credit facility).
 • Mfano kama umepewa tenda ya kusupply Mifuko 1000 ya mbolea kwenda kampuni X ya kilimo, Basi ukiwa na kampuni yako ni rahisi kampuni Y inayozalisha Mbolea hizo kukupa mzigo mbolea ukasupply kwa mteja X; na wewe ukawalipa baada ya kupewa hela. (Yaani unatumia mtaji wa manufacturer wewe kufanya biashara hata kama huna mtaji).
 • Ukiwa umesajili kampuni unakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kupata ushirikiano na hao walengwa wako kwa haraka zaidi maana wanakuwa wanaongea na kampuni na sio mtu binafsi. hii ni Kama una wazo la kutafuta wafadhili wa biashara yako.
 • Kuna makato madogo ya kodi kwasababu kampuni unakatwa kodi kiasi cha faida ulichoshindwa kutumia na sio kiasi cha mauzo yote. Yaani unakatwa kodi baada ya matumizi na sio kabla ya matumizi.
 • Mfano: Kama una mauzo ya Milioni 100; basi ambaye hana kampuni atakatwa zaidi ya Milioni 10 au zaidi. Lakini  kampuni unakatwa kodi kiasi cha faida tu ambacho hujatumia. Yaani kama kwenye mauzo ya Milioni 100 ulikuwa na faida ya Milioni 30;  lakini ukaitumia hiyo faida kwa matumizi ya kampuni (Mfano kununua gari ya kampuni, kuwekeza, n.k) baadaye ukabaki na Milioni 5, basi unakatwa kodi kwenye hiyo Milioni 5. Kitu ambacho hakipo kwa Mtu binafSi.
 • Chini ya kampuni moja unaweza kufanya biashara nyingi tofauti, ili linawezekana kupitia kukata leseni tofauti za biashara (business license) kulingana na shughuli unazotaka kufanya. Yaani kampuni moja inaweza kuwa na leseni za biashara zaidi ya moja.
 • Ukiwa na kampuni ni rahisi kumrithisha ndugu, mtoto au mtu wako wa karibu hizo biashara kupitia hiyo kampuni. Ukifanya biashara kama mtu binafsi inamaanisha wewe ndiyo mmiliki pekee wa hiyo biashara, yaani hautaweza kummilikisha mtu mwingine.
 • Pia unakuwa na nafasi ya kutofautisha mali zako binafsi na mali za kampuni. Hii itakusaidia pale ambapo imetokea kampuni yako inadaiwa, basi deni hilo halitafika kwenye mali zako binafsi ambazo hazimilikiwi na kampuni

UNAHITAJI KUFUNGUA KAMPUNI?

  USAJILI WA KAMPUNI

 • Chagua jina la kampuni
 • Sanduku la posta
 • Mkoa, wilaya, kata, Mtaa, Jirani na kitu gani maarufu.
 • Director A awe amefikisha miaka 21, Nida namba, Email, Namba ya simu, Tin namba kama huna omba online bure hapa https://ots.tra.go.tz/
 • Director B,C, D jaza taarifa kama Director A
 • Wanahisa (Nida namba, Email, Namba ya simu)
 • Hisa idadi na mgawanyo wake
 • Orodhesha shughuli zote mnazotarajia kuzifanya na kampuni yako

NB Maandalizi yanafanywa ndani ya siku moja ya kazi kutokana na foleni ya maombi ya awali (kuandaa memorandum na nyaraka za usajili)

HUDUMA  ZETU.

 • Kufanikisha usajili wa kampuni yako na jina la biashara Tanzania
 • Kufanikisha Usajili wa Trademark ya biashara yako
 • Kuupdate kampuni yako, au kufanya mabadiloko yoyote
 • Kutengeneza Company profile, logo.
 • Kuandaa Business Plan
 • Kutoa Mafunzo ya Uendeshaji wa kampuni

Wasiliana nasi 0715561595 kupata huduma kwa bei nafuu

Leave A Comment

Related Posts

MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WAHITIMU WA VYUO VYA ELIMU YA JUU

“Badili Changamoto  kuwa Fursa” Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es  Salaam anawatangazia   wahitimu wote wa elimu ya juu kuwa Chuo Kikuu  cha Dar es Salaam kimeandaa   mafunzo  ya ujasiriamali yatakayotolewa  katika mikoa kumi  na moja ya Tanzania  (Tanzania Bara na Zanzibar) mwezi  Oktoba na Novemba mwaka 2021.  Mafunzo haya yanatolewa  kama sehemu  ya huduma  kwa […]

NAFASI ZA KAZI DYNAMIC HIGH SCHOOL

Dynamic High School yenye Matawi Dar es Salaam na Mbeya imetangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo 1. HEADMASTER Awe na digrii ya ualimu kutoka chuo chochote kinachotambulika na serikali, uzoefu usiopungua miaka mitatu kwenye uongozi wa shule za sekondari na awe na umri usiozidi miaka 45. 2.SECRETARY WA SHULE Awe na certificate au diploma ya usecretary kutoka […]

Mabalozi, MyvodacomApp & Mpesa App

Vodacom Tanzania wakishirikiana na Unipromo Tanzania wanakuja na kampeni ya Mpesa App na Myvodacom app ili kuwafikishia wateja urahisi wa kufanya miamala na kununua vifurushi. Kampeni imeanza kwa wanavyuo vikuu na vyuo vya kati kote nchini ili kuhamasisha jamii kurahisisha maisha kupitia  Aplikesheni salama ya Vodacom na Mpesa Historia Fupi ya Uni Balozi Vodacom Tanzania kwa mara […]