MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WAHITIMU WA VYUO VYA ELIMU YA JUU

“Badili Changamoto  kuwa Fursa”

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es  Salaam anawatangazia   wahitimu wote wa elimu ya juu kuwa Chuo Kikuu  cha Dar es Salaam kimeandaa   mafunzo  ya ujasiriamali yatakayotolewa  katika mikoa kumi  na moja ya Tanzania  (Tanzania Bara na Zanzibar) mwezi  Oktoba na Novemba mwaka 2021.  Mafunzo haya yanatolewa  kama sehemu  ya huduma  kwa jamii inayofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

LENGO  KUU LA MAFUNZO                        

Kuwapatia  vijana  uelewa,  taarifa, maarifa, ujuzi na uwezo  wa  kuainisha  fursa zinazowazunguka na kuweza  kuzitumia  fursa hizo kwa kuanzisha  biashara  na kutoa ajira kwa ajili yao na wenzao na hivyo kuboresha maisha yajamii kwa ujumla.

MALENGO  MAHUSUSI

 • Kujenga  uwezo na tabia ya kutumia  taaluma  zao kutambua matatizo na changamoto kama fursa za kibiashara.
 • Kukutana  na kujifunza  kutoka kwa wajasiriamali  wazoefu kutoka kwenye sekta mbalimbali.
 • Kutengeneza mipango ya  biashara ambayo itawasaidia kutafuta mitaji.
 • Kuwaunganisha vijana   wenye   mawazo   mazun   ya ujasiriamali na  watoa huduma za  kifedha, teknolojia na uatamizi.

WALENGWA

Mafunzo haya yanawalenga   vijana wahitimu wa Vyuo vya
Elimu ya Juu kuanzia Diploma wenye nia ya kujiajiri.

MUDA WAMAFUNZO

Mafunzo haya yatatolewa katika makundi ya watu wasiozidi 50 kwa darasa kwa muda wa siku nne mfululizo.

RA TIBA YA MAFUNZO

#Mahali                   Tarehe  za Mafunzo           Mwishowa Kujisajili
1Dar es Salaam      04/10/2021    – 14/10/2021        29/09/2021
2Morogoro              06/10/2021    – 14/10/2021          29/09/2021
3Mtwara                    06/10/2021    – 14/10/2021           29/09/2021
4Tanga 06/10/2021 – 14/10/2021 29/09/2021
5Dodoma18/10/2021 –  21/10/202113/10/2021
6Kigoma18/10/2021 –    21/10/202113/10/2021
7Mjini Magharibi 18/10/2021 –  21/10/202113/10/2021
8Geita20/10/2021 – 28/10/202115/10/2021
9Kilimanjaro25/10/2021 –  28/10/202120/10/2021
10Njombe25/10/2021 – 28/10/202120/10/2021
11Kusini Pemba 01/11/2021 – 04/11/2021 28/10/2021

GHARAMA  ZA MAFUNZO

Washiriki hawatalipa  ada. Wanaotoka mbali watajigharamia usafiri wa kwenda na kurudi na malazi.

JINSI YA KUSHIRIKI

Kujisajili, tembelea tovuti ya Chuo Kikuu cha DSM na kujaza maombi kwa kupitia fomu iliyo katika tovuti ya  http://udsm-mafunzo.ac.tz

Kwa changamoto yoyote wasiliana nasi kwa kutuma barua pepe kwenye anuani udiec@udsm.ac. tz na/au WhatsApp no. +255-734-669-818.

Kwa Mawasiliano zaidi:

Mkurugenzi,  Kitengo cha Ubunifu na Ujasiriamali  (UDIEC)

s.L.P 110099 Dar es Salaam

Tel: +255-734-669-818 +255-758-461-028.

Email: udiec@udsm.ac.tz.

“WAHl  KUJIANDIKISHA  NAFASI NI CHACHE”

4 Comments

 1. Bado transcript hazijatoka kwa wanafunzi wa mwaka huu, kwaajili ya kuaplod kwenye fumu ya kushiriki, Naona kama kuna cheti kingine chochote kinaweza wekwa kama mmbadala

 2. 14 September 2021
  MARIAM JUMA KHATIB
  Reply

  Napendekeza kuwe na cheti cha ushiriki na mafunzo ya vitendo

Leave A Comment

Related Posts

NAFASI ZA KAZI DYNAMIC HIGH SCHOOL

Dynamic High School yenye Matawi Dar es Salaam na Mbeya imetangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo 1. HEADMASTER Awe na digrii ya ualimu kutoka chuo chochote kinachotambulika na serikali, uzoefu usiopungua miaka mitatu kwenye uongozi wa shule za sekondari na awe na umri usiozidi miaka 45. 2.SECRETARY WA SHULE Awe na certificate au diploma ya usecretary kutoka […]

Usajili Biashara Brela (Jina/Kampuni)

A. JINA LA BIASHARA  (BUSINESS NAME) Kuna utofauti kati ya kampuni na jina la biashara (business name). Jina la biashara ni jina la utambulisho ambalo umeamua biashara yako ifahamike na kuitwa. Mfano ni majina ambayo wengi wanaandika kwenye maduka yao. Yale ni majina ambayo wameamua duka na biashara zao zitambulike Hivyo. Business name ni jina tu la […]

Mabalozi, MyvodacomApp & Mpesa App

Vodacom Tanzania wakishirikiana na Unipromo Tanzania wanakuja na kampeni ya Mpesa App na Myvodacom app ili kuwafikishia wateja urahisi wa kufanya miamala na kununua vifurushi. Kampeni imeanza kwa wanavyuo vikuu na vyuo vya kati kote nchini ili kuhamasisha jamii kurahisisha maisha kupitia  Aplikesheni salama ya Vodacom na Mpesa Historia Fupi ya Uni Balozi Vodacom Tanzania kwa mara […]